Tuesday, February 10, 2015

AZAM FC KUING'OA KILELENI YANGA SC LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA.

 Azam Fc

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Azam itacheza na wanatamtam Mtibwa Sugar Jumatano hii katika jitihada za kuiondoa kileleni mwa ligi, klabu ya Yanga.

Azam, baada ya kutoka sare ya 2-2 na Polisi Morogoro katika mchezo iliopita, inahitaji pointi tatu muhimu ili kufikisha pointi 25, kuwa kileleni sawa na Yanga.
Yanga ilifanikiwa kuwa kileleni mwa ligi kuu ya timu 14 baada ya kuifunga Mtibwa Sugar 2-0 katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juma lililopita.


Afisa habari wa azam yenye maskani yake katika uwanja wa chamazi complex jijini dar es alaam, Jaffar Idi Mwana wa Maganga ameiambia Mpenja Blog kuwa hawapo tayari kupoteza pointi tatu muhimu katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Mtibwa.
"Hatupo tayari kabisa kuona kunapoteza pointi tatu muhimu dhidi ya klabu ya Mtibwa kwani makosa tuliyoyafanya dhidi ya polisi morogoro tumeyafanyia kazi, na tutahakikisha tunaibuka na ushindi katika mchezo huo," alisema Jaffar Idi.
Mtibwa Sugar
 
Endapo kama Mtibwa watafanikiwa kuwafunga Azam, Mtibwa ikiwa chini ya kocha Mecky Mexime, nahodha wa zamani wa timu ya taifa (Taifa Stars),itafikisha pointi 21.

 Mtibwa ilishawahi kuwa mabingwa wa Tanzania Bara mara mbili mfululizo, mwaka 1999-2000 huku Azam ikiwa ni mabingwa mara moja katika msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment